Mungu wetu umekuwa ni Mungu asiyeweza kufananishwa na kiumbe kingine chochote duniani ,hii ni Kwa sababu ya maajabu makubwa ayatendayo yasiyoelezeka Kwa urahisi Kwa akiri zetu za kibinadamu ,amekuwa akitembea na wanadamu kizazi hadi kizazi akiwafunulia mambo ambayo hayanabudi kutokea kabla hayajaleta maafa kwao kitu ambacho kinaendelea kumtofautisha kabisa na viumbe vingine ,hivyo Kwa namna ya pekee kabisa amezungumza na wazazi wetu wa kwanza moja Kwa moja hapo kabla ya dhambi ,kisha akaongea nao Kwa njia ya waamuzi,wafalme na manabii Kwa nyakati tofauti tofauti ,hadi leo anazungumza nasi pia Kwa njia ya neno lake ambalo alitumia hao hao manabii na wafalme katika kuriwasilisha Kwa viumbe wake kama sisi ,Kwa kupitia maono,mafunuo neno la unabii likatufikia ,hivi karibuni tutaanza kujifunza unabii kuanzia sura ya kwanza ya Kitabu cha Daniel mpaka sura ya kumi na mbili ,kisha tutaendelea na Kitabu cha ufunuo kuanzia sura ya kwanza hadi ya 22 ,kwahiyo ninawaarika sana muendelee kufuatilia masomo haya yatawasaidia sio tu katika kutambua maisha haya yalivyo bali pia kutambua ya kwamba nikwa namna gani maisha haya yanaenda kubadirishwa kabisa ,kaa tayari kufahamu nani anayabadirisha ,je yanaelekea kuharibika au kuboreshwa huu ndio unabii ,unakuja kukupa mwanga ,mahali usipofahamu kuhusu maisha yako utafahamu bila shida kabisa muombe Mungu tunapoanza unabii akuongoze uelewe vizuri, lakini pia usisite kuuliza swali ,kutoa maoni na kuwashirikisha wengine pia utayapata masomo yote hapa hapa.
Unabii wa biblia ,sehemu Ya Kwanza.
Reviewed by Unknown
on
April 07, 2018
Rating:
Naomba masomo ya unabii kuhusu Daniel na ufunuo
ReplyDelete