Ninakukaribisha sana rafiki mpendwa wa masomo ya unabii na mfuatiliaji wa hii application ya mjue sana Mungu kwa hakika ukiwa tayari utamjua kwelikweli ,Tunaanza Kitabu cha Danieli kama nilivyokudokezea hapo awali hiki kitabu kinahusu nyakati zetu hizi za mwisho. Hivyo Kuelewa mambo yaliyo mbele yetu ni muhimu sana,kama wasafiri yatupasa kujua mwanga wetu na namna hasa mambo yanavyoendelea kwa njia hii tutapata kujua ama tutapata uzima wa milele, ama mauti ya milele katika mkabala wetu na matukio hayo yanayokuja. Hivyo si suala dogo kujifunza unabii wa kitabu cha Danieli kwa wote wanaotaka uzima wa milele. Tukijikumbusha wakati Yesu akizungumza na wanafunzi wake juu ya matukio ya siku za mwisho alisema, "Basi hapo mtakapoliona Chukizo la Uharibifu, lile lililonenwa na Danieli, limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu)". Mathayo 24:15. Ninakuomba tuanze kwanza na hii hatua uangalie Kwa makini hasa maana ya maneno haya " chukizo la uharibifu" Pia kumbuka kwamba katika haya yote kuna hatari kubwa mbele yetu! Yesu anataka kila asomaye alifahamu Chukizo hilo la Uharibifu linalokuja ili atakapoliona akimbie kuokoa maisha yake (Mt. 24:16-22). Chukizo la Uharibifu limetajwa mahali patatu katika kitabu cha Danieli (Dan. 9:26,27; 11:31; 12:11). Mpendwa msomaji hili chukizo la uharibifu Lina majina mengi katika kitabu cha Danieli na cha Ufunuo----- Pembe Ndogo, Mnyama, na kadhalika. Utashangaa kujua kwamba "mnyama" katika lugha ya taaluma ya unabii sio tusi wala kashfa kama wengi wanavyodhani. Maana yake ni "mfalme au ufalme" (Dan.7:17)kama tutakavyoona Kwa upana katika sura hii tukiifikia. Biblia inajitafsiri yenyewe! Hivi maana ya
"chukizo" ni nini?
Soma 2 Wafalme 21:1-11 na Kumbukumbu la Torati 18:9-14. Kumbe! Chukizo ni kuabudu sanamu, kuwaomba wafu, kushughulika na mapepo, uchawi au ushirikina, kuabudu jua na nyota za mbinguni, na kadhalika. Mataifa, yaani, wapagani hufanya mambo hayo.
Je! "uharibifu" ni nini?
Sio kuharibu vitu, bali ni kuwaangamiza, yaani, kuwaua watu (Dan.8:24,25).
Kwa hiyo, Chukizo la Uharibifu ni mamlaka au utawala au ufalme unaoabudu sanamu, unaowaomba wafu, ulio na ushirikina, na, zaidi ya hayo, unaowaangamiza "watakatifu",
Lakini pia tuangalie watakatifu ni watu gani , "hao wazishikao Amri [Kumi] za Mungu na Imani ya Yesu (Ufu.14:12; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12).
Pia nyakati za Paulo aliliona hili chukizo ndio maana analiita "mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu [mwuaji], mpingamizi [au Mpinga Kristo]
(2 The. 2:3,4].
Bila shaka umeanza kupata picha hasa juu ya haya maneno, kila mtu atapata kumjua huyo mpinga Kristo, kabla Yesu Kristo hajarudi (tutajifunza zaidi hapo mbele) hapa duniani. Tutaendelea kusumbuka na magonjwa, umaskini, na dhiki mpaka atakapokuja mwokozi wetu baada ya huyo mwana wa kuasi kutokea.
Je! si jambo la muhimu kabisa kuijua mamlaka hiyo ili kujua la kufanya kuokoa maisha yetu, si yale ya kimwili, bali ya kiroho ili tupate kuishi milele? (Mt. 10:26-33; Yoh.6:39-40; Ufu.12:11). Kufa au kutokufa si hoja, bali kujiweka tayari kumlaki Yesu Kristo atakapokuja juu ya mawingu ya mbinguni (Ufu. 2:10; Mt. 24:29-31).
Mpendwa Msomaji, je! kwa neema yake Mungu unataka kuwa tayari kujiunga na watakatifu ulimwenguni kote? Hao wazishikao amri na imani ya yesu ,Somo la Amri litatolewa ndani ya masomo haya utaelewa vizuri, je, unataka kujifunza zaidi unabii wa biblia ,usipate shaka Karibu na endelea kufuatilia ukurasa huu wa masomo ya unabii ,kumbuka Kabla hujaanza kusoma somo, omba ili Mungu akupe Roho wake atakayekufundisha kweli yote (Yohana 16:13-15). Mungu na akubariki! Mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa unabii huu .
Karibu Kwa kuanza sura ya kwanza ya Kitabu cha Daniel.

Unabii Sehemu Ya Pili.
Reviewed by Unknown
on
April 10, 2018
Rating:
No comments: